Skip to content
الأنعَام /

Aya 40

6 : 40
الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 40

قُلۡ أَرَءَيۡتَكُمۡ إِنۡ أَتَىٰكُمۡ عَذَابُ ٱللَّهِ أَوۡ أَتَتۡكُمُ ٱلسَّاعَةُ أَغَيۡرَ ٱللَّهِ تَدۡعُونَ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ

Sema: Mwaonaje ikikujieni adhabu ya Mwenyezi Mungu, au ikakufikieni hiyo Saa - mtamwomba asiye kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi ni wakweli?

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Waambie hawa makafiri: Nambieni, ikikujieni adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani, au ikikujieni Kiyama kwa vitisho vyake, mtamuelekea yeyote asiye kuwa Mwenyezi Mungu mkimnyenyekea wakati huo akufaeni kwa lolote, kama nyinyi mnasema kweli katika kumuabudu kwenu asiye kuwa Mwenyezi Mungu?