Skip to content
الأنعَام /

Aya 28

6 : 28

Aya 28 of الأنعَام (6 : 28). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 28

بَلۡ بَدَا لَهُم مَّا كَانُواْ يُخۡفُونَ مِن قَبۡلُۖ وَلَوۡ رُدُّواْ لَعَادُواْ لِمَا نُهُواْ عَنۡهُ وَإِنَّهُمۡ لَكَٰذِبُونَ

Bali yamewadhihirikia waliyo kuwa wakiyaficha zamani. Na kama wangeli rudishwa bila ya shaka wange yarejea yale yale waliyo katazwa. Na hakika hao ni waongo.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kauli yao hii haikuwa ila kwa kuwa haimkiniki tena kuficha wala kufanya ukaidi katika yale anayo waambia Mtume. Na lau kama wakirudishwa duniani wataurejea tena ukafiri alio wakataza Mwenyezi Mungu. Haya ni kwa ghururi zao kughurika na mapambo ya dunia, na kwa kufuata kwao matamanio yao. Na hakika hao wanasema uwongo kwa kudai kuwa wataamini pindi wakirejeshwa duniani.