6 : 27
وَلَوۡ تَرَىٰٓ إِذۡ وُقِفُواْ عَلَى ٱلنَّارِ فَقَالُواْ يَٰلَيۡتَنَا نُرَدُّ وَلَا نُكَذِّبَ بِـَٔايَٰتِ رَبِّنَا وَنَكُونَ مِنَ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
Na unge ona watakapo simamishwa kwenye Moto, wakawa wanasema: Laiti tungeli rudishwa, wala hatutakanusha tena Ishara za Mola wetu Mlezi, na tutakuwa miongoni wa Waumini.
Explanation & meanings · 1
- Ewe Nabii! Lau ungeli waona hawa makafiri, watavyo simama mbele ya Moto wakisononeka na vitisho vyake, ungeli ona jambo la ajabu lenye kutisha, nao wanatamani warejeshwe tena duniani, wakisema: Laiti tungeli rudishwa duniani tukatengeneza tuliyo yaharibu! Wala hatutakanusha Ishara za Mola wetu Mlezi. Na tutakuwa miongoni wa Waumini.