6 : 23
ثُمَّ لَمۡ تَكُن فِتۡنَتُهُمۡ إِلَّآ أَن قَالُواْ وَٱللَّهِ رَبِّنَا مَا كُنَّا مُشۡرِكِينَ
Kisha hautakuwa udhuru wao ila ni kusema: Wallahi! Mola wetu Mlezi! Hatukuwa washirikina.
Explanation & meanings · 1
- Kisha hayatakuwa matokeo ya hayo matatizo yao magumu pahala hapo ila kujitoa kimaso-maso kutokana na ushirikina wao kwa kusema uwongo. Waseme: Wallahi Mola Mlezi wetu! Hatukumshirikisha nawe yeyote katika ibada.