6 : 22
وَيَوۡمَ نَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشۡرَكُوٓاْ أَيۡنَ شُرَكَآؤُكُمُ ٱلَّذِينَ كُنتُمۡ تَزۡعُمُونَ
Siku tutapo wakusanya wote pamoja, kisha tuwaambie walio shirikisha: Wako wapi washirikishwa wenu mlio kuwa mnadai?
Explanation & meanings · 1
- Na watajie yatakayo tokea Siku tutapo kusanya viumbe vyote kwa ajili ya hisabu. Kisha tutawaambia kwa kuwahizi walio kuwa wakiwaabudu wenginewe pamoja na Mwenyezi Mungu: Wako wapi mlio wafanya ni washirika wa Mwenyezi Mungu, wapate kukufaeni?