Skip to content
الأنعَام /

Aya 108

6 : 108

Aya 108 of الأنعَام (6 : 108). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الأنعَام Aya 165
Sura · الأنعَام
Kiswahili · Barawani
6 : 108

وَلَا تَسُبُّواْ ٱلَّذِينَ يَدۡعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ فَيَسُبُّواْ ٱللَّهَ عَدۡوَۢا بِغَيۡرِ عِلۡمٖۗ كَذَٰلِكَ زَيَّنَّا لِكُلِّ أُمَّةٍ عَمَلَهُمۡ ثُمَّ إِلَىٰ رَبِّهِم مَّرۡجِعُهُمۡ فَيُنَبِّئُهُم بِمَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ

Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyo kuwa wakiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi Waumini! Msiyatukane masanamu ya washirikina wanayo yaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, isije chuki yao kwa hayo ikawapelekea hasira ya kumtukana Mwenyezi Mungu kwa uadui na ujinga. Kama tulivyo wapambia hawa kupenda masanamu yao, kila umma una a'mali yake kwa mujibu wa makdara yao. Na marejeo ya wote ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake Siku ya Kiyama. Naye atawaeleza khabari ya vitendo vyao, na atawalipa kwavyo.