Skip to content
المَائدة /

Aya 96

5 : 96

Aya 96 of المَائدة (5 : 96). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 96

أُحِلَّ لَكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَحۡرِ وَطَعَامُهُۥ مَتَٰعٗا لَّكُمۡ وَلِلسَّيَّارَةِۖ وَحُرِّمَ عَلَيۡكُمۡ صَيۡدُ ٱلۡبَرِّ مَا دُمۡتُمۡ حُرُمٗاۗ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ ٱلَّذِيٓ إِلَيۡهِ تُحۡشَرُونَ

Nyinyi mmehalalishiwa kuvua vinyama vya baharini na kuvila, kwa faida yenu na kwa wasafiri. Na mmeharimishiwa mawindo ya wanyama wa bara maadamu mmeharimia Hija. Na mcheni Mwenyezi Mungu ambaye mtakusanywa kwake.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu amekuhalalishieni kuvua wanyama wa baharini, na muwale, na wanufaike kwao wakaazi wenyeji na wasafiri. Na amekuharimishieni kuwinda wanyama wa bara wasio fugwa kwa kawaida majumbani, katika muda ule unapo kuwa katika Hija au Umra, kwenye eneo takatifu linalo itwa Alharam. Na mzingatieni Mwenyezi Mungu, na iogopeni adhabu yake. Basi msende kinyume naye, kwani nyinyi mtarejea kwake Siku ya Kiyama, na hapo atakulipeni kwa yote mliyo yatenda. (Huu ni mfano katika mifano mingi ya Uislamu tangu hapo kale unavyo pendelea kulinda tabia ya mazingara kwa kuhifadhi wanyama wasiuliwe ovyo, na miti isikatwe ovyo, na hata maji ya mito na maziwa yasitumiwe kwa fujo, kwani Mwenyezi Mungu hawapendi wafujaji!)