Skip to content
المَائدة /

Aya 71

5 : 71

Aya 71 of المَائدة (5 : 71). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 71

وَحَسِبُوٓاْ أَلَّا تَكُونَ فِتۡنَةٞ فَعَمُواْ وَصَمُّواْ ثُمَّ تَابَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ ثُمَّ عَمُواْ وَصَمُّواْ كَثِيرٞ مِّنۡهُمۡۚ وَٱللَّهُ بَصِيرُۢ بِمَا يَعۡمَلُونَ

Na wakadhani kuwa hapatakuwa majaribio; basi wakawa vipofu na viziwi. Kisha Mwenyezi Mungu akawapokelea toba zao. Kisha tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona hayo wayatendayo.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hao Wana wa Israili walidhani hawatapata majaribio, yaani shida za kuwafafanua baina ya walio simama imara na wasio simama imara. Kwa hivyo hawakuweza kustahamili, bali wengi wao walipotea wakawa kama vipofu na viziwi. Wakaiacha Haki, na Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa madhila. Baadae walipo rejea kwa Mwenyezi Mungu na wakatubu, alikubali toba zao, na akawarejeshea utukufu wao. Lakini baadae tena wakaingia katika upotofu, na wakawa kama vipofu na viziwi! Na Mwenyezi Mungu anawajua vyema, na atashuhudia vitendo vyao, na atawalipa kwavyo.