Skip to content
المَائدة /

Aya 46

5 : 46

Aya 46 of المَائدة (5 : 46). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 46

وَقَفَّيۡنَا عَلَىٰٓ ءَاثَٰرِهِم بِعِيسَى ٱبۡنِ مَرۡيَمَ مُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِۖ وَءَاتَيۡنَٰهُ ٱلۡإِنجِيلَ فِيهِ هُدٗى وَنُورٞ وَمُصَدِّقٗا لِّمَا بَيۡنَ يَدَيۡهِ مِنَ ٱلتَّوۡرَىٰةِ وَهُدٗى وَمَوۡعِظَةٗ لِّلۡمُتَّقِينَ

Na tukawafuatishia hao Isa bin Maryamu kuyahakikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na tukampa Injili iliyomo ndani yake uwongofu, na nuru na inayo sadikisha yaliyo kuwa kabla yake katika Taurati, na uwongofu na mawaidha kwa wachamngu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na baada ya hawa Manabii tulimtuma Isa mwana wa Maryamu, naye ni mwenye kufuata njia yao, na kuithibitisha Taurati iliyo mtangulia. Naye tulimteremshia Injili yenye uwongofu kuelekea Haki, na yenye kubainisha hukumu, na tuliiteremsha ili isadikishe Taurati iliyo tangulia, na ndani yake pana uwongofu wa kupelekea Haki, na ni mawaidha kwa wachamngu. (Tazama Injili ya Mathayo 5.17 maneno ya Nabii Isa: "Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.")