Skip to content
المَائدة /

Aya 40

5 : 40

Aya 40 of المَائدة (5 : 40). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 40

أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ لَهُۥ مُلۡكُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضِ يُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ وَيَغۡفِرُ لِمَن يَشَآءُۗ وَٱللَّهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٞ

Hujui ya kwamba Mwenyezi Mungu anao ufalme wa mbingu na ardhi? Humuadhibu amtakaye, na humsamehe amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.

Explanation & meanings · 1
  1. Jua, ewe mwenye fahamu, kwa ujuzi wa yakini, ya kwamba ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kumiliki kila kitu kiliomo katika mbingu na ardhi. Yeye humpa adhabu yake amtakaye, kwa hikima yake na uwezo wake. Na humsamehe amtakaye, kwa hikima yake na rehema yake. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.