Skip to content
المَائدة /

Aya 11

5 : 11

Aya 11 of المَائدة (5 : 11). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

المَائدة Aya 120
Sura · المَائدة
Kiswahili · Barawani
5 : 11

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱذۡكُرُواْ نِعۡمَتَ ٱللَّهِ عَلَيۡكُمۡ إِذۡ هَمَّ قَوۡمٌ أَن يَبۡسُطُوٓاْ إِلَيۡكُمۡ أَيۡدِيَهُمۡ فَكَفَّ أَيۡدِيَهُمۡ عَنكُمۡۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَۚ وَعَلَى ٱللَّهِ فَلۡيَتَوَكَّلِ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ

Enyi mlio amini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yenu, walipo taka watu kukunyooshieni mikono, naye akaizuilia mikono yao kukufikieni. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi Waumini! Kumbukeni neema za Mwenyezi Mungu juu yenu katika wakati wa shida, pale baadhi ya Washirikina walipo kusudia kukuuweni nyinyi na Mtume wenu, Mwenyezi Mungu akazuia balaa yao isikufikieni, na akakuokoeni. Shikamaneni na kumcha Mwenyezi Mungu, na mumtegemee Yeye peke yake, katika mambo yenu. Kwani Yeye anakutosheni. Inavyo muelekea Muumini ni kumtegemea Mwenyezi Mungu peke yake daima milele.