Skip to content
Al-Ma'idah /

Aya 101

5 : 101

Aya 101 of Al-Ma'idah (5 : 101). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Al-Ma'idah Aya 120
Sura · Al-Ma'idah
Kiswahili · Barawani
5 : 101

يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَا تَسۡـَٔلُواْ عَنۡ أَشۡيَآءَ إِن تُبۡدَ لَكُمۡ تَسُؤۡكُمۡ وَإِن تَسۡـَٔلُواْ عَنۡهَا حِينَ يُنَزَّلُ ٱلۡقُرۡءَانُ تُبۡدَ لَكُمۡ عَفَا ٱللَّهُ عَنۡهَاۗ وَٱللَّهُ غَفُورٌ حَلِيمٞ

Enyi mlio amini! Msiulize mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni. Na mkiyauliza inapo teremshwa Qur'ani mtabainishiwa. Mwenyezi Mungu amesamehe hayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira Mpole.

Explanation & meanings · 1
  1. Enyi mlio amini! Msimuulize Nabii mambo ambayo Mwenyezi Mungu amekuficheni mkataka yafichuliwe, na mkamuuliza Nabii katika uhai wake, kwani Qur'ani inamteremkia bado. Na Mwenyezi Mungu atakubainishieni itapo hitajika. Mwenyezi Mungu amekusameheni kwa yasiyo tajwa, hatokuadhibuni kwayo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye wasaa katika upole. Basi hana papara katika kuadhibu.