Skip to content
مُحمد /

Aya 16

47 : 16

Aya 16 of مُحمد (47 : 16). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

مُحمد Aya 38
Sura · مُحمد
Kiswahili · Barawani
47 : 16

وَمِنۡهُم مَّن يَسۡتَمِعُ إِلَيۡكَ حَتَّىٰٓ إِذَا خَرَجُواْ مِنۡ عِندِكَ قَالُواْ لِلَّذِينَ أُوتُواْ ٱلۡعِلۡمَ مَاذَا قَالَ ءَانِفًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ وَٱتَّبَعُوٓاْ أَهۡوَآءَهُمۡ

Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza, mpaka wakiondoka kwako huwauliza walio pewa ilimu: Amesema nini sasa hivi? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amepiga muhuri juu ya nyoyo zao, na wakafuata pumbao lao.

Explanation & meanings · 1
  1. Na miongoni mwa makafiri kipo kikundi cha watu wanao kusikiliza wewe, Muhammad. Hawakuamini wewe, wala hawanafiiki na maneno yako. Mpaka wakisha ondoka kwenye baraza yako husema kwa kejeli kuwaambia walio pewa ujuzi: Kasema nini huyu Muhammad sasa hivi? Watu hao ndio Mwenyezi Mungu amepiga muhuri wa ukafiri juu ya nyoyo zao. Ndio wameiacha kheri wakifuata matamanio yao.