Skip to content
الأحقَاف /

Aya 24

46 : 24
الأحقَاف Aya 35
Sura · الأحقَاف
Kiswahili · Barawani
46 : 24

فَلَمَّا رَأَوۡهُ عَارِضٗا مُّسۡتَقۡبِلَ أَوۡدِيَتِهِمۡ قَالُواْ هَٰذَا عَارِضٞ مُّمۡطِرُنَاۚ بَلۡ هُوَ مَا ٱسۡتَعۡجَلۡتُم بِهِۦۖ رِيحٞ فِيهَا عَذَابٌ أَلِيمٞ

Basi walipo liona wingu likielekea kwenye mabonde yao, walisema: Wingu hili la kutunyeshea mvua! Kumbe sivyo, haya ni hayo mliyo yahimiza, upepo ambao ndani yake imo adhabu chungu!

Explanation & meanings · 1
  1. Ikawajia adhabu kwa sura ya wingu. Walipo liona limetanda kote juu linaelekea mabondeni kwao, walisema kwa furaha: Wingu hili linatuletea mvua na kheri. Wakaambiwa: Bali hilo ni hayo mliyo yahimiza, nayo ni upepo wenye adhabu kali na chungu, itakayo teketeza kila kitu kwa amri ya Muumbaji wake. Nao ukawaangamiza, yasionekane mabaki yao isipo kuwa nyumba zao. Hivyo ndivyo tunavyo mlipa kila mwenye kutenda kama makosa yao.