46 : 13
إِنَّ ٱلَّذِينَ قَالُواْ رَبُّنَا ٱللَّهُ ثُمَّ ٱسۡتَقَٰمُواْ فَلَا خَوۡفٌ عَلَيۡهِمۡ وَلَا هُمۡ يَحۡزَنُونَ
Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu; kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu, wala hawatahuzunika.
Explanation & meanings · 1
- Hakika wanao sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu peke yake, kisha wakatengenea kwa kufanya vitendo vizuri, watu hao hawana khofu ya kushukiwa la karaha, na wala hawatahuzunika kwa kuyakosa wayatakayo.