Skip to content
الأحقَاف /

Aya 11

46 : 11
الأحقَاف Aya 35
Sura · الأحقَاف
Kiswahili · Barawani
46 : 11

وَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لِلَّذِينَ ءَامَنُواْ لَوۡ كَانَ خَيۡرٗا مَّا سَبَقُونَآ إِلَيۡهِۚ وَإِذۡ لَمۡ يَهۡتَدُواْ بِهِۦ فَسَيَقُولُونَ هَٰذَآ إِفۡكٞ قَدِيمٞ

Na walio kufuru waliwaambia walio amini: Lau kuwa hii ni kheri, wasingeli tutangulia. Na walipo kosa kuongoka wakasema: Huu ni uzushi wa zamani.

Explanation & meanings · 1
  1. Na walio kufuru walisema kuwakhusu walio amini, kwa kejeli na majivuno juu yao: Ingeli kuwa aliyo kuja nayo Muhammad ni ya kheri, basi wasingeli tutangulia hawa katika kuyaamini. Kwani sisi ndio twenye ubwana, na akili bora! Na ilivyo kuwa hawakuyafuata basi wakaangukia kuyatoa kombo, wakisema: Huu ni uwongo wa zamani unatokana na hadithi za watu wa kale!