43 : 49
وَقَالُواْ يَٰٓأَيُّهَ ٱلسَّاحِرُ ٱدۡعُ لَنَا رَبَّكَ بِمَا عَهِدَ عِندَكَ إِنَّنَا لَمُهۡتَدُونَ
Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.
Explanation & meanings · 1
- Wakasema, kumlilia Musa balaa zilipo waenea: Ewe mchawi - ndio Mwanachuoni kikwao - Tuombee kwa Mola wako Mlezi, kwa kutawasali na ahadi yake aliyo kupa, atuondolee adhabu hii! Hakika sisi tukifarijiwa bila ya shaka tutaongoka.