43 : 36
وَمَن يَعۡشُ عَن ذِكۡرِ ٱلرَّحۡمَٰنِ نُقَيِّضۡ لَهُۥ شَيۡطَٰنٗا فَهُوَ لَهُۥ قَرِينٞ
Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea Shet'ani kuwa ndiye rafiki yake.
Explanation & meanings · 1
- Na mwenye kujitia upofu na Qur'ani aliyo iteremsha Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema kuwa ni kumbusho kwa walimwengu wote, tunamsalitisha na Shetani, anakuwa naye daima, akimpoteza na akimzuzua.