4 : 71
يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ خُذُواْ حِذۡرَكُمۡ فَٱنفِرُواْ ثُبَاتٍ أَوِ ٱنفِرُواْ جَمِيعٗا
Enyi mlio amini! Chukueni hadhari yenu! Na mtoke kwa vikosi au tokeni nyote pamoja!
Explanation & meanings · 1
- Enyi Mlio amini! Daima kuweni na hadhari na maadui wenu. Jizatitini kupambana na vitimbi vyao. Na mkitoka kwenda vitani tokeni kwa vikosi vikosi, au tokeni nyote pamoja.