Skip to content
النِّسَاء /

Aya 162

4 : 162

Aya 162 of النِّسَاء (4 : 162). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النِّسَاء Aya 176
Sura · النِّسَاء
Kiswahili · Barawani
4 : 162

لَّٰكِنِ ٱلرَّٰسِخُونَ فِي ٱلۡعِلۡمِ مِنۡهُمۡ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ يُؤۡمِنُونَ بِمَآ أُنزِلَ إِلَيۡكَ وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبۡلِكَۚ وَٱلۡمُقِيمِينَ ٱلصَّلَوٰةَۚ وَٱلۡمُؤۡتُونَ ٱلزَّكَوٰةَ وَٱلۡمُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ أُوْلَٰٓئِكَ سَنُؤۡتِيهِمۡ أَجۡرًا عَظِيمًا

Lakini walio bobea katika ilimu miongoni mwao, na Waumini, wanayaamini uliyo teremshiwa wewe, na yaliyo teremshwa kabla yako. Na wanao shika Swala, na wakatoa Zaka, na wanao muamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho - hao tutawapa malipo makubwa.

Explanation & meanings · 1
  1. Lakini walio bobea katika ilimu, yaani wataalamu kweli kweli, miongoni mwa Mayahudi, na Waumini katika umma wako, Ewe Nabii, wanasadiki wahyi ulio funuliwa wewe, na walio letewa Mitume wa kabla yako. Na wanao shika Swala baraabara, na wanatoa Zaka, na wanamuamini Mwenyezi Mungu na kufufuliwa na hisabu, hao Mwenyezi Mungu atawalipa malipo mema kabisa kwa imani yao na ut'iifu wao.