39 : 1
تَنزِيلُ ٱلۡكِتَٰبِ مِنَ ٱللَّهِ ٱلۡعَزِيزِ ٱلۡحَكِيمِ
Mteremsho wa Kitabu hiki umetokana na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
Explanation & meanings · 1
- Qur'ani imeteremka kutokana na Mwenyezi Mungu, ambaye hana wa kumshinda kwa atakayo; Mwenye hikima katika vitendo vyake na utungaji wa sharia zake.