37 : 99
وَقَالَ إِنِّي ذَاهِبٌ إِلَىٰ رَبِّي سَيَهۡدِينِ
Na akasema: Hakika mimi nahama, nakwenda kwa Mola wangu Mlezi; Yeye ataniongoa.
Explanation & meanings · 1
- Ibrahim alipo kata tamaa nao, kuwa hawaamini tena, alisema: Mimi ninahama kwendea pahala alipo niamrisha Mola wangu Mlezi nende. Mola wangu Mlezi atanihidi aniongoze mpaka nifike pahala pa utulivu, penye amani, na nchi nzuri.