Skip to content
فَاطِر /

Aya 44

35 : 44

Aya 44 of فَاطِر (35 : 44). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

فَاطِر Aya 45
Sura · فَاطِر
Kiswahili · Barawani
35 : 44

أَوَلَمۡ يَسِيرُواْ فِي ٱلۡأَرۡضِ فَيَنظُرُواْ كَيۡفَ كَانَ عَٰقِبَةُ ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِهِمۡ وَكَانُوٓاْ أَشَدَّ مِنۡهُمۡ قُوَّةٗۚ وَمَا كَانَ ٱللَّهُ لِيُعۡجِزَهُۥ مِن شَيۡءٖ فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَلَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنَّهُۥ كَانَ عَلِيمٗا قَدِيرٗا

Je! Hawakusafiri katika ardhi wakaona vipi ulikuwa mwisho wa walio kuwa kabla yao? Na hao walikuwa wana nguvu zaidi kuliko wao. Na hapana kitu kinacho weza kumshinda Mwenyezi Mungu mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye kujua, Mwenye uweza.

Explanation & meanings · 1
  1. Je! hao hukaa na wakakanya tu ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina, bila ya wao kusafiri katika ulimwengu wakaangalia kwa macho yao athari za maangamizo yaliyo wateremkia walio kuwa kabla yao kwa sababu ya kuwakadhibisha kwao Mitume? Na kabla ya wao yalikuwako mataifa yaliyo kuwa na nguvu kushinda wao. Nguvu zao hazikuweza kuzuia adhabu ya Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye hashindwi na chochote kilioko mbinguni wala katika ardhi. Hakika Yeye ni Mwenye ilimu kubwa kabisa, Mwenye uweza mkubwa kabisa.