35 : 15
۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ أَنتُمُ ٱلۡفُقَرَآءُ إِلَى ٱللَّهِۖ وَٱللَّهُ هُوَ ٱلۡغَنِيُّ ٱلۡحَمِيدُ
Enyi watu! Nyinyi ndio wenye haja kwa Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa.
Explanation & meanings · 1
- Enyi watu! Nyinyi ndio mnao mhitajia Mwenyezi Mungu kwa kila kitu. Na Yeye Mwenyezi Mungu peke yake ndiye Mwenye kujitosha, hawahitajii viumbe vyake. Na Yeye ndiye Mwenye kustahiki kusifiwa kwa kila hali