28 : 41
وَجَعَلۡنَٰهُمۡ أَئِمَّةٗ يَدۡعُونَ إِلَى ٱلنَّارِۖ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ لَا يُنصَرُونَ
Na tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Kiyama hawatanusuriwa.
Explanation & meanings · 1
- Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: Na tukawafanya hao ni wenye kuitia watu kwenye ukafiri, ambao khatima yake ni Moto. Na Siku ya Kiyama hawampati wa kuwanusuru na kuwatoa kwenye adhabu.