Skip to content
النور /

Aya 50

24 : 50

Aya 50 of النور (24 : 50). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

النور Aya 64
Sura · النور
Kiswahili · Barawani
24 : 50

أَفِي قُلُوبِهِم مَّرَضٌ أَمِ ٱرۡتَابُوٓاْ أَمۡ يَخَافُونَ أَن يَحِيفَ ٱللَّهُ عَلَيۡهِمۡ وَرَسُولُهُۥۚ بَلۡ أُوْلَٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّٰلِمُونَ

Je! Wana maradhi katika nyoyo zao, au wanaona shaka, au wanaogopa ya kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake watawadhulumu? Bali hao ndio madhaalimu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na kwa nini wanasimama msimamo huu katika kushitakiana mbele ya Mtume? Ni kwa sababu nafsi zao zimesibiwa na maradhi ya upofu, na kwa hivyo haziridhiki na hukumu yako ya haki? Au ni kwa kuwa wao wanatilia shaka uadilifu wa Muhammad s.a.w. katika kuhukumu? Si lolote katika hayo kabisa. Lakini hao ni madhaalimu walio dhulumu nafsi zao na wengineo kwa sababu ya ukafiri wao na unaafiki wao na kuiacha kwao haki.