Skip to content
النور /

Aya 47

24 : 47
النور Aya 64
Sura · النور
Kiswahili · Barawani
24 : 47

وَيَقُولُونَ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَبِٱلرَّسُولِ وَأَطَعۡنَا ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٞ مِّنۡهُم مِّنۢ بَعۡدِ ذَٰلِكَۚ وَمَآ أُوْلَٰٓئِكَ بِٱلۡمُؤۡمِنِينَ

Na wanasema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tumet'ii. Kisha kikundi katika hao hugeuka baada ya hayo. Wala hao si wenye kuamini.

Explanation & meanings · 1
  1. Na wanaafiki husema kwa ndimi zao: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na Mtume, na tunazifuata amri zao. Na wanapo tiwa mtihanini kikundi kati yao hukataa kushirikiana na Waislamu katika kazi ya kheri, kama Jihadi na nyenginezo, baada ya kauli yao hii. Na watu hawa si Waumini wa kweli, wala hawastahiki kutumiliwa jina la Waumini kwao.