Skip to content
البَقَرَة /

Aya 9

2 : 9

Aya 9 of البَقَرَة (2 : 9). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 9

يُخَٰدِعُونَ ٱللَّهَ وَٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ وَمَا يَخۡدَعُونَ إِلَّآ أَنفُسَهُمۡ وَمَا يَشۡعُرُونَ

Wanatafuta kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walio amini, lakini hawadanganyi ila nafsi zao; nao hawatambui.

Explanation & meanings · 1
  1. Hao makafiri wadanganyifu huwakhadaa Waumini kwa wanayo yafanya, na wao hudhania kuwa wanamdanganya Mwenyezi Mungu. Wanafikiri kuwa Yeye hayajui wanayo yaficha, na kumbe Yeye anayajua ya siri na yanayo non'gonwa. Basi wao kwa hakika wanajikhadaa wenyewe, kwa sababu madhara ya vitendo vyao yatawapata wao, sasa au baadae. Mwenye kumkhadaa mtu, na akadhani kuwa huyo mtu hajui naye kumbe anajua, basi inakuwa anajikhadaa mwenyewe nafsi yake.