2 : 42
وَلَا تَلۡبِسُواْ ٱلۡحَقَّ بِٱلۡبَٰطِلِ وَتَكۡتُمُواْ ٱلۡحَقَّ وَأَنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
Wala msichanganye kweli na uwongo na mkaificha kweli nanyi mnajua.
Explanation & meanings · 1
- Wala msichanganye Haki iliyo toka kwangu na upotovu mlio uzua nyinyi, hata ikawa halijuulikani la kweli na la uwongo. Wala msiifiche Haki, na katika hiyo Haki ni kumsadiki Muhammad, na nyinyi mnajua kuwa yeye ni wa kweli na wa kusadikiwa.