Skip to content
البَقَرَة /

Aya 248

2 : 248

Aya 248 of البَقَرَة (2 : 248). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 248

وَقَالَ لَهُمۡ نَبِيُّهُمۡ إِنَّ ءَايَةَ مُلۡكِهِۦٓ أَن يَأۡتِيَكُمُ ٱلتَّابُوتُ فِيهِ سَكِينَةٞ مِّن رَّبِّكُمۡ وَبَقِيَّةٞ مِّمَّا تَرَكَ ءَالُ مُوسَىٰ وَءَالُ هَٰرُونَ تَحۡمِلُهُ ٱلۡمَلَٰٓئِكَةُۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَةٗ لَّكُمۡ إِن كُنتُم مُّؤۡمِنِينَ

Na Nabii wao akawaambia: Alama ya ufalme wake ni kukuleteeni lile sanduku ambalo mna ndani yake kituliza nyoyo zenu, kitokacho kwa Mola wenu Mlezi, na mna mabaki ya waliyo yaacha kina Musa na kina Harun, wanalichukua Malaika. Bila shaka katika hayo zimo dalili kwenu ikiwa nyinyi mnaamini.

Explanation & meanings · 1
  1. Na Nabii wao aliwaambia: "Hakika dalili ya ukweli wangu kuwa Mwenyezi Mungu amemteua Twaluti awe ni mtawala wenu ni kuwa atakurejesheeni sanduku la Taurati mlio nyang'anywa, linalo bebwa na Malaika. Na ndani yake yamo baadhi ya mabaki ya watu wa Musa na watu wa Harun walio kuja baada yao. Na likiletwa sanduku hilo nyoyo zenu zitatua. Katika hayo hakika pana dalili ambazo zitakupelekeeni kumfuata na kumridhia, ikiwa kama kweli nyinyi mnataka Haki na mnaiamini."