Skip to content
البَقَرَة /

Aya 230

2 : 230

Aya 230 of البَقَرَة (2 : 230). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 230

فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُۥ مِنۢ بَعۡدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوۡجًا غَيۡرَهُۥۗ فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيۡهِمَآ أَن يَتَرَاجَعَآ إِن ظَنَّآ أَن يُقِيمَا حُدُودَ ٱللَّهِۗ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوۡمٖ يَعۡلَمُونَ

Na kama amempa t'alaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwengine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayo ibainisha kwa watu wanao jua.

Explanation & meanings · 1
  1. Mume akimwacha mkewe mara ya tatu baada ya T'alaka mbili za mwanzo basi hamhalalikii mpaka yule mke aolewe na mume mwengine aingie harusi. Akimwacha baada ya hapo basi anaweza kufunga ndoa tena na yule mume wa kwanza, na wala hapana dhambi juu yao kuanza maisha mapya kwa ndoa mpya. Lakini yawapasa waazimie kuendesha maisha mema ya mume na mke wakifuata sharia alizo ziwekea mipaka Mwenyezi Mungu Subhanahu wa Taa'la. Na mipaka hii imebainishwa wazi kwa mwenye kuamini sharia ya Kiislamu na anataka ilimu na a'mali njema.