Skip to content
البَقَرَة /

Aya 17

2 : 17

Aya 17 of البَقَرَة (2 : 17). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 17

مَثَلُهُمۡ كَمَثَلِ ٱلَّذِي ٱسۡتَوۡقَدَ نَارٗا فَلَمَّآ أَضَآءَتۡ مَا حَوۡلَهُۥ ذَهَبَ ٱللَّهُ بِنُورِهِمۡ وَتَرَكَهُمۡ فِي ظُلُمَٰتٖ لَّا يُبۡصِرُونَ

Mfano wao ni kama mfano wa aliye koka moto, na ulipo tanda mwangaza wake kote kote Mwenyezi Mungu aliiondoa nuru yao na akawawacha katika giza, hawaoni.

Explanation & meanings · 1
  1. Hali ya watu hawa katika unaafiki wao ni kama hali ya mwenye kuwasha moto apate nafuu yeye na watu wake. Moto ukisha waka ukatoa mwangaza kunawiri kote, Mwenyezi Mungu huwaondolea Nuru wenye kuwasha wakawa katika giza zito, hawaoni chochote. Kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwatunukia sababu za kuongoka, nao hawakuzishika. Kwa hivyo macho yao yakazibwa, wakastahiki kubaki katika kuemewa na upotovu.