Skip to content
البَقَرَة /

Aya 106

2 : 106

Aya 106 of البَقَرَة (2 : 106). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

البَقَرَة Aya 286
Sura · البَقَرَة
Kiswahili · Barawani
2 : 106

۞ مَا نَنسَخۡ مِنۡ ءَايَةٍ أَوۡ نُنسِهَا نَأۡتِ بِخَيۡرٖ مِّنۡهَآ أَوۡ مِثۡلِهَآۗ أَلَمۡ تَعۡلَمۡ أَنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيۡءٖ قَدِيرٌ

Ishara yoyote tunayo ifuta au tunayo isahaulisha tunailetea iliyo bora kuliko hiyo, au iliyo mfano wake. Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu?

Explanation & meanings · 1
  1. Nao walikutaka wewe Muhammad, uwaletee miujiza, ishara, ile waliokuja nayo Musa na Manabii wa Wana wa Israili. Sisi yatutosha kuwa tumekutia nguvu kwa kukuletea Qur'ani. Na Sisi tunapo acha nguvu kumpa Nabii anaye kuja nyuma kwa muujiza wa Nabii aliye tangulia, au tukawasahaulisha watu athari za muujiza ule, basi Sisi humletea huyu Nabii aliyekuja baadaye muujiza, kuwa ni Ishara, au Aya, iliyo bora zaidi au mfano wa ile ili kuwa ni dalili ya ukweli wake. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. (Na hapana Ishara, Muujiza au Aya, iliyo kubwa na bora na yenye kudumu kuliko hii Qur'ani.)