Skip to content
الكَهف /

Aya 34

18 : 34

Aya 34 of الكَهف (18 : 34). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الكَهف Aya 110
Sura · الكَهف
Kiswahili · Barawani
18 : 34

وَكَانَ لَهُۥ ثَمَرٞ فَقَالَ لِصَٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُۥٓ أَنَا۠ أَكۡثَرُ مِنكَ مَالٗا وَأَعَزُّ نَفَرٗا

Naye alikuwa na mazao mengi. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu!

Explanation & meanings · 1
  1. Na huyo mwenye vitalu alikuwa na mali mengine yenye kutoa mazao yake pia. Basi ikamuingia ghururi kwa neema ile. Katika ile ghururi yake akamwambia mwenzie yule Muumini nao walikuwa wakijadiliana: Mimi nina mali mengi kuliko wewe, na ninakushinda kwa nguvu za jamaa zangu na wasaidizi.