17 : 63
قَالَ ٱذۡهَبۡ فَمَن تَبِعَكَ مِنۡهُمۡ فَإِنَّ جَهَنَّمَ جَزَآؤُكُمۡ جَزَآءٗ مَّوۡفُورٗا
Akasema Mwenyezi Mungu: Ondokelea mbali! Atakaye kufuata katika wao, basi Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yenu, malipo ya kutimia.
Explanation & meanings · 1
- Mola akamwambia kwa kumtisha na kumlegezea kamba: Endelea na shani yako uliyo jichagulia kuifuata. Atakaye kut'ii wewe katika wana wa Adam, basi Jahannamu itakuwa ndiyo malipo yako na yao, malipo ya kutosha yaliyo kamilika.