Skip to content
الإسرَاء /

Aya 61

17 : 61
الإسرَاء Aya 111
Sura · الإسرَاء
Kiswahili · Barawani
17 : 61

وَإِذۡ قُلۡنَا لِلۡمَلَٰٓئِكَةِ ٱسۡجُدُواْ لِأٓدَمَ فَسَجَدُوٓاْ إِلَّآ إِبۡلِيسَ قَالَ ءَأَسۡجُدُ لِمَنۡ خَلَقۡتَ طِينٗا

Na pale tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam. Wakamsujudia isipo kuwa Iblisi. Akasema: Je! Nimsujudie uliye muumba kwa udongo?

Explanation & meanings · 1
  1. Na Mwenyezi Mungu anakumbusha asli ya kuumba na uadui baina ya mwanaadamu na Iblisi, pale alipo waambia Malaika: Msujudieni Adam kwa kumuamkia na kumhishimu kwa kumuinamia. Hapo hapo wakasujudu. Isipo kuwa Iblisi akakataa, na akasema kwa chuki: Vipi nimsujudie uliye muumba kwa udongo, na hali mimi umeniumba kwa moto. Mimi ni bora kuliko yeye.