17 : 111
وَقُلِ ٱلۡحَمۡدُ لِلَّهِ ٱلَّذِي لَمۡ يَتَّخِذۡ وَلَدٗا وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ شَرِيكٞ فِي ٱلۡمُلۡكِ وَلَمۡ يَكُن لَّهُۥ وَلِيّٞ مِّنَ ٱلذُّلِّۖ وَكَبِّرۡهُ تَكۡبِيرَۢا
Na sema: Alhamdulillah, Himdi zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye hana mwana, wala hana mshirika katika ufalme, wala hana rafiki wa kumsaidia kwa sababu ya udhaifu wake. Na mtukuze kwa utukufu mkubwa.
Explanation & meanings · 1
- Nasema Alhamdulillah, Himdi zote, yaani sifa na shukrani, ni za Mwenyezi Mungu ambaye hakuzaa mwana, kwani hamhitajii; wala hana mshirika katika ufalme, kwani Yeye peke yake ndiye aliye uanzisha; wala hana msaidizi wa kumtia nguvu kwa udhaifu fulani unao mpata. Na mtukuze Mola wako Mlezi kwa utukufu mkubwa ulio laiki naye.