Skip to content
الرَّعد /

Aya 43

13 : 43

Aya 43 of الرَّعد (13 : 43). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

الرَّعد Aya 43
Sura · الرَّعد
Kiswahili · Barawani
13 : 43

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ لَسۡتَ مُرۡسَلٗاۚ قُلۡ كَفَىٰ بِٱللَّهِ شَهِيدَۢا بَيۡنِي وَبَيۡنَكُمۡ وَمَنۡ عِندَهُۥ عِلۡمُ ٱلۡكِتَٰبِ

Na walio kufuru wanasema: Wewe hukutumwa. Sema: Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi baina yangu na nyinyi, na pia yule mwenye ilimu ya Kitabu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na hadi ya ushindani wao hao wanao kanya na hawaikubali Haki ni kukwambia: Ewe Nabii! Wewe si Mtume aliye toka kwa Mwenyezi Mungu! Basi waambie: Yanitosha mimi kuwa Mwenyezi Mungu ndiye wa kunihukumia mimi nanyi, na anaye ijua hakika ya Qur'ani na ajabu zake za miujiza ya kushangaza inayo ingia katika akili ziliyo nzima.