Skip to content
الرَّعد /

Aya 21

13 : 21
الرَّعد Aya 43
Sura · الرَّعد
Kiswahili · Barawani
13 : 21

وَٱلَّذِينَ يَصِلُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيَخۡشَوۡنَ رَبَّهُمۡ وَيَخَافُونَ سُوٓءَ ٱلۡحِسَابِ

Na wale ambao huyaunga aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanaikhofu hisabu mbaya.

Explanation & meanings · 1
  1. Hao ni Waumini; ada yao ni mapenzi na ut'iifu. Hao wanaamini mapendo baina ya watu, na wanahurumia jamaa zao, na wanawasaidia wenzi wao katika Haki, na wao wanaijua Haki ya Mwenyezi Mungu, na wanaiogopa hisabu ya kuwachusha Siku ya Kiyama, na kwa hivyo wanajikinga na madhambi kwa kadri wawezavyo.