11 : 74
فَلَمَّا ذَهَبَ عَنۡ إِبۡرَٰهِيمَ ٱلرَّوۡعُ وَجَآءَتۡهُ ٱلۡبُشۡرَىٰ يُجَٰدِلُنَا فِي قَوۡمِ لُوطٍ
Basi khofu ilipo mwondoka Ibrahim, na ikawa ile bishara imemfikia, alianza kujadiliana nasi juu ya kaumu ya Lut'.
Explanation & meanings · 1
- Zilipo mtoka khofu Ibrahim, na akaisikia bishara ya kumfurahisha ya kupata mwana, ikamwingia huruma, akaanza kujadiliana na wale wajumbe katika shauri la kuangamizwa kaumu Lut'.