Skip to content
هُود /

Aya 64

11 : 64

Aya 64 of هُود (11 : 64). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 64

وَيَٰقَوۡمِ هَٰذِهِۦ نَاقَةُ ٱللَّهِ لَكُمۡ ءَايَةٗۖ فَذَرُوهَا تَأۡكُلۡ فِيٓ أَرۡضِ ٱللَّهِۖ وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوٓءٖ فَيَأۡخُذَكُمۡ عَذَابٞ قَرِيبٞ

Enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu ni Ishara kwenu. Basi mwacheni ale katika ardhi ya Mwenyezi Mungu; wala ms!imguse kwa ubaya, isije ikakuangamizeni adhabu iliyo karibu.

Explanation & meanings · 1
  1. Na enyi watu wangu! Huyu ngamia wa Mwenyezi Mungu; amemfanya awe ni alama kwenu ya kushuhudia ukweli wa haya ninayo kuleteeni. Kwani huyu ni namna mbali na hao mlio wazoea. Basi mwachieni ale katika ardhi ya Mwenyezi, kwani yeye ni ngamia wake, na ardhi ni yake. Wala msimfikishie uovu wowote wa kumdhuru. Kwani mkifanya hivyo Mwenyezi Mungu atakuangamizeni kwa adhabu iliyo karibu.