Skip to content
هُود /

Aya 63

11 : 63

Aya 63 of هُود (11 : 63). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 63

قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي مِنۡهُ رَحۡمَةٗ فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِنۡ عَصَيۡتُهُۥۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيۡرَ تَخۡسِيرٖ

Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake - je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamtanizidishia ila khasara tu.

Explanation & meanings · 1
  1. Akasema: Enyi watu wangu! Hebu nambieni: ikiwa mimi kwa haya ninayo kukuitieni kwayo nina ujuzi nayo vilivyo, na nina hoja za kunitia nguvu kutoka kwa Mola wangu Mlezi, na ikawa Mola wangu Mlezi kanipa mimi na nyinyi rehema itokayo kwake, nayo ni Unabii na Utume, vipi basi nende kinyume na amri yake, na nimuasi kwa kutofikisha ujumbe wake kwa sababu ya kukusikilizeni nyinyi? Na nani wa kuninusuru na kunisaidia kuikinga adhabu yake nikimuasi Yeye? Nyinyi hamwezi kuninusuru na kunikinga na adhabu yake. Basi hamtonizidishia ila kupotea na kuingia khasarani ni kikut'iini nyinyi, na nikamuasi Mola wangu na Mola wenu Mlezi.