Skip to content
هُود /

Aya 42

11 : 42

Aya 42 of هُود (11 : 42). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 42

وَهِيَ تَجۡرِي بِهِمۡ فِي مَوۡجٖ كَٱلۡجِبَالِ وَنَادَىٰ نُوحٌ ٱبۡنَهُۥ وَكَانَ فِي مَعۡزِلٖ يَٰبُنَيَّ ٱرۡكَب مَّعَنَا وَلَا تَكُن مَّعَ ٱلۡكَٰفِرِينَ

Ikawa inakwenda nao katika mawimbi kama milima. Na Nuhu akamwita mwanawe naye alikuwa mbali: Ewe mwanangu! Panda pamoja nasi, wala usiwe pamoja na makafiri.

Explanation & meanings · 1
  1. Wakaingia katika Safina, ikawa inakwenda katika mawimbi makubwa makubwa kama milima! Na ilipo anza kwenda Nuhu alimkumbuka mwanawe kwa huruma ya baba, naye alikuwa yuko mbali kajitenga na wito wa baba yake. Akamwita: Ewe mwanangu! Panda nasi, wala usiwe katika wanao ikataa Dini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu!