Skip to content
هُود /

Aya 36

11 : 36

Aya 36 of هُود (11 : 36). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

هُود Aya 123
Sura · هُود
Kiswahili · Barawani
11 : 36

وَأُوحِيَ إِلَىٰ نُوحٍ أَنَّهُۥ لَن يُؤۡمِنَ مِن قَوۡمِكَ إِلَّا مَن قَدۡ ءَامَنَ فَلَا تَبۡتَئِسۡ بِمَا كَانُواْ يَفۡعَلُونَ

Na akafunuliwa Nuhu akaambiwa: Hataamini yeyote katika watu wako ila wale walio kwisha amini. Basi usisikitike kwa waliyo kuwa wakiyatenda.

Explanation & meanings · 1
  1. Mwenyezi Mungu akamletea wahyi Nuhu akamwambia: Hatakusadiki wala hataifuata Haki yeyote katika kaumu yako baada ya sasa, isipo kuwa wale walio kwisha tangulia kukuamini kabla ya hayo. Basi ewe Nuhu! Usihuzunike kwa sababu ya waliyo kuwa wakikutendea, ya kukukadhibisha, na kukuudhi. Kwani Sisi tutawalipiza karibu.