11 : 35
أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ إِنِ ٱفۡتَرَيۡتُهُۥ فَعَلَيَّ إِجۡرَامِي وَأَنَا۠ بَرِيٓءٞ مِّمَّا تُجۡرِمُونَ
Au ndio wanasema: Ameizua? Sema: Ikiwa nimeizua, basi kosa hilo ni juu yangu, na mimi sikhusiki na makosa myatendayo.
Explanation & meanings · 1
- Nini msimamo wa washirikina kukhusu hadithi hizi za kweli? Watasema kazizua? Wakisema hivyo, basi waambie: Ikiwa nimezizua kama mnavyo dai, basi hilo ni kosa kubwa; ni juu yangu mimi tu dhambi zake! Na ikiwa nimesema kweli, basi nyinyi ndio wenye makosa, na mimi sikhusiki na matokeo ya makosa yenu.