Skip to content
Hud /

Aya 120

11 : 120

Aya 120 of Hud (11 : 120). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

Hud Aya 123
Sura · Hud
Kiswahili · Barawani
11 : 120

وَكُلّٗا نَّقُصُّ عَلَيۡكَ مِنۡ أَنۢبَآءِ ٱلرُّسُلِ مَا نُثَبِّتُ بِهِۦ فُؤَادَكَۚ وَجَآءَكَ فِي هَٰذِهِ ٱلۡحَقُّ وَمَوۡعِظَةٞ وَذِكۡرَىٰ لِلۡمُؤۡمِنِينَ

Na yote tunayo kusimulia katika khabari za Mitume ni ya kukupa nguvu moyo wako. Na katika haya imekujia haki na mawaidha na ukumbusho kwa Waumini.

Explanation & meanings · 1
  1. Ewe Nabii! Tunakusimulia kila namna ya khabari ya Mitume walio pita pamoja na kaumu zao kwa ajili ya kukupa nguvu wewe uweze kubeba mashaka ya Utume. Na katika khabari hizi yamekujia maelezo ya haki unayo ilingania mfano walivyo lingania Mitume walio kutangulia, nayo ni Tawhidi ya kuwa Mwenyezi Mungu ni Mpweke, na kuepuka yale ambayo yanamkasirisha, kama yalivyo wajia mawaidha na mazingatio yanayo wanufaisha Waumini, ili wazidi imani yao, na wanao jitayarisha kwa imani ili waifanyie haraka hiyo imani.