Skip to content
يُونس /

Aya 99

10 : 99

Aya 99 of يُونس (10 : 99). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 99

وَلَوۡ شَآءَ رَبُّكَ لَأٓمَنَ مَن فِي ٱلۡأَرۡضِ كُلُّهُمۡ جَمِيعًاۚ أَفَأَنتَ تُكۡرِهُ ٱلنَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُواْ مُؤۡمِنِينَ

Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?

Explanation & meanings · 1
  1. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka watu wote katika ardhi waamini, wangeli amini. Basi wewe usihuzunike kwa ukafiri wa washirikina. Wala haiwi Imani ila kwa khiari. Basi wewe huwezi kuwalazimisha watu kwa nguvu ili wafuate Haki na waitikie. Haikupasii kutaka kuwalazimisha waamini, wala hutoweza, hata ukijitahidi vipi.