10 : 85
فَقَالُواْ عَلَى ٱللَّهِ تَوَكَّلۡنَا رَبَّنَا لَا تَجۡعَلۡنَا فِتۡنَةٗ لِّلۡقَوۡمِ ٱلظَّٰلِمِينَ
Wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu.
Explanation & meanings · 1
- Waumini wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu peke yake. Kisha wakamwomba Mola wao Mlezi asiwatie katika mitihani na mateso ya makafiri.