Skip to content
يُونس /

Aya 78

10 : 78

Aya 78 of يُونس (10 : 78). This page carries the verse in the Uthmani script with a translation of its meaning, at a stable URL that can be cited on its own.

يُونس Aya 109
Sura · يُونس
Kiswahili · Barawani
10 : 78

قَالُوٓاْ أَجِئۡتَنَا لِتَلۡفِتَنَا عَمَّا وَجَدۡنَا عَلَيۡهِ ءَابَآءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا ٱلۡكِبۡرِيَآءُ فِي ٱلۡأَرۡضِ وَمَا نَحۡنُ لَكُمَا بِمُؤۡمِنِينَ

Wakasema: Je! Umetujia ili utuachishe tuliyo wakuta nayo baba zetu, na mpate nyinyi wawili ukubwa katika nchi? Wala sisi hatukuaminini nyinyi.

Explanation & meanings · 1
  1. Firauni na watu wake walimwambia Musa: Hapana shaka wewe umekuja kwa makusudi ya kutuachisha dini ya baba zetu, na mila za kaumu yetu, ili nyinyi wawili mpate kuwa na wafuasi; wewe na nduguyo mpate ufalme na utukufu na urais wa kutawala na kuhukumu! Kwa hivyo basi sisi hatutakuaminini nyinyi wala huo utume wenu!