Skip to content
839 Hadithi

Ensaiklopidia ya Hadithi za Nabii

Chuja matokeo

Kadi 116 kati ya 839

Ondoa vichujio

Msimulizi

Onyesha wasimulizi wote (57)
Nilisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni kupi kunusurika? Akasema: "Shika ulimi wako, na ikutoshe nyumba yako, na lia kwa ajili ya makosa yako".
Sahihi Imepokelewa na Tirmidhiy na Ahmad
"Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)".
Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyinginezo Imepokelewa na Ahmad
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Assalaam alaikum, akamjibu, kisha akakaa, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kumi" Kisha akaja mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaah, akamjibu, akakaa, akasema: "Ishirini" Kisha akaja mtu mwingine akasema: Assalaam alaikum warahmatullaahi wabarakaatuh, akamjibu akakaa, akasema: "Thelathini".
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud na Tirmidhiy, Ahmad na Ad-Darimi
"Hakuna mtu yeyote atakayetenda dhambi, kisha akasimama akajitwaharisha, kisha akaswali, kisha akamuomba Allah msamaha, isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe", Kisha akasoma aya hii: "Na wale ambao wakifanya machafu au wakizidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakaomba msamaha kutokana na madhambi yao" [Al-Imran: 135].
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na Ahmad
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimuona mtu mmoja akiswali peke yake nyuma ya safu, akamuamrisha arudie swala yake.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani katika Maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi, wakasema: Basi tukajifunza elimu na kuifanyia kazi.
Ni nzuri (Hasan) Imepokelewa na Ahmad
"Hakuna ndoa ila kuwe na walii (Msimamizi)".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na Ahmad
"Atakayechukua elimu katika elimu ya unajimu basi atakuwa kajichukulia sehemu ya uchawi, atazidi kuwa mchawi mkubwa kila anavyozidi kujifunza uchawi".
Sahihi Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na Ahmad